Acts 13:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miaka 450 ilipita, halafu akawapatia waamuzi wawaongoze mpaka wakati wa nabii Samueli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya yote yalichukua kama muda wa miaka mia nne na hamsini. “Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi hadi wakati wa nabii Samweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
baada ya hayo akawapa waamuzi hata zamani za nabii Samweli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yote haya yalitokea katika kipindi cha kadiri ya miaka mia nne na hamsini. Baada ya hili, Mungu akawapa watu wetu waamuzi kuwaongoza mpaka wakati wa nabii Samweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Miaka mia nne na hamsini ilipita, halafu akawapatia waamuzi wawaongoze mpaka wakati wa nabii Samweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miaka 450 ilipita, halafu akawapatia waamuzi wawaongoze mpaka wakati wa nabii Samueli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya yote yalichukua kama muda wa miaka 450. “Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi mpaka wakati wa nabii Samweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya yote yalichukua kama muda wa miaka 450. “Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi mpaka wakati wa nabii Samweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
baada ya hayo akawapa waamuzi hata wakati wa nabii Samweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miaka 450 ilipita, halafu akawapatia waamuzi wawaongoze mpaka wakati wa nabii Samueli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawapa waamuzi miaka kama 450, mpaka siku za mfumbuaji Samueli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
baada ya hayo akawapa waamuzi hata zamani za nabii Samweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mambo haya yote yalitendeka kwa muda wa miaka yapata mia ine makumi tano. “Kisha akawapa waamuzi kwa kuwaongoza mpaka katika siku za nabii Samweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baada ya muda wa miaka aruba mia na khamsini, akawapa waamuzi hatta zamani za nabii Samwil.