Acts 13:26 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ndugu, nyinyi mlio watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wengine wote mnaomcha Mungu! Ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ndugu zangu, wana wa Ibrahimu, nanyi watu wa Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu zangu, wana katika familia ya Ibrahimu na ninyi watu wengine ambao pia mnamwabudu Mungu wa kweli, sikilizeni! Habari kuhusu wokovu huu imeletwa kwetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ndugu, ninyi mlio watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wengine wote mnaomcha Mungu! Ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ndugu, nyinyi mlio watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wengine wote mnaomcha Mungu! Ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ndugu zangu, wana wa Abrahamu, nanyi watu Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ndugu zangu, wana wa Ibrahimu, nanyi watu wa Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Abrahamu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ndugu, nyinyi mlio watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wengine wote mnaomcha Mungu! Ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waume ndugu zangu, wana wa uzao wa Aburahamu, nanyi mnaomcha Mungu, Neno la wokovu huu lilitumwa kufika kwetu sisi;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Wandugu zangu, ninyi wazao wa Abrahamu na ninyi watu wa mataifa mengine munaokuwa hapa kwa kumwabudu Mungu, habari hii ya wokovu imetumwa kwetu!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, nao miongoni mwenu mnaomcha Mungu, kwenu ninyi neno la wokofu huu limepelekwa.