Acts 13:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho wa Mungu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini hadi kisiwa cha Kipro.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Barnaba na Sauli walitumwa na Roho Mtakatifu. Walikwenda katika mji wa Seleukia. Kutoka hapo walitweka tanga na kusafiri mpaka kwenye kisiwa cha Kipro.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho Mtakatifu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho wa Mwenyezi Mungu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi watu hao, walipotumwa hadi Kipro na Roho Mtakatifu wakateremkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hivyo, walivyotumwa na Roho Mtakatifu, wakatelemka kwenda Seleukia; huko wakaingia chomboni kwenda Kipuro.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Barnaba na Saulo wakaenda kwenye kivuko cha Seleukia kwa uongozi wa Roho Mutakatifu. Kule wakaingia ndani ya chombo na kwenda mpaka katika kisanga cha Kipuro.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Selukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hatta Kupro.