Acts 13:45 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Wayahudi walipoona umati ule mkubwa wa watu, walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wayahudi waliokuwepo pale walipowaona watu wote hawa, wakaingiwa na wivu sana. Wakakashifu na kubishia kila kitu alichosema Paulo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Wayahudi walipoona ule umati mkubwa wa watu walijawa na wivu na kunena maneno ya kashfa kuhusu yale Paulo aliyokuwa akisema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Wayahudi walipoona ule umati mkubwa wa watu walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Wayuda walipoyaona hayo makundi ya watu wakajazwa wivu, wakayabisha yaliyosemwa na Paulo na kumtukana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wayuda walipoona lile kundi la watu, wakajaa na wivu sana, nao wakapinga maneno Paulo aliyosema na kumutukana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.