Acts 13:48 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uhai wa milele, wakawa waumini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Mwenyezi Mungu; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wasio Wayahudi waliposikia Paulo akisema hivi, walifurahi sana. Waliuheshimu ujumbe wa Bwana, na wengi wao wakauamini. Hawa ni wale waliochaguliwa kuupata uzima wa milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uzima wa milele, wakawa waumini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uhai wa milele, wakawa waumini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana Isa; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uhai wa milele, wakawa waumini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wamizimu walipoyasikia haya wakafurahi, wakalitukuza Neno la Bwana, wakalitegemea wote waliokuwa wamewekewa kupata uzima wa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati watu wa mataifa mengine waliposikia maneno haya wakafurahi, wakatukuza neno la Bwana. Nao wote waliokuwa wamechaguliwa kwa kupata uzima wa milele, wakaamini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.