Acts 13:50 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake wa tabaka ya juu wa mataifa mengine ambao walikuwa wacha Mungu, na wanaume maarufu wa mji huo. Wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba, wakawafukuza kutoka katika eneo lao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini viongozi wa Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka eneo hilo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Wayahudi pale walisababisha baadhi ya wanawake muhimu waifuatayo dini na viongozi wa mji kuwakasirikia na kuwachukia Paulo na Barnaba na wakawafukuza mjini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake wa tabaka ya juu wa mataifa mengine ambao walikuwa wacha Mungu, na wanaume maarufu wa mji huo. Wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba, wakawafukuza kutoka katika eneo lao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake wa tabaka ya juu wa mataifa mengine ambao walikuwa wacha Mungu, na wanaume maarufu wa mji huo. Wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba, wakawafukuza kutoka katika eneo lao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka kwenye eneo lao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka eneo hilo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake wa tabaka ya juu wa mataifa mengine ambao walikuwa wacha Mungu, na wanaume maarufu wa mji huo. Wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba, wakawafukuza kutoka katika eneo lao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Wayuda waliwachokoza wanawake wakuu walioyashika matambiko yao, hata wakubwa wa mji, wakawachukua, wawashambulie akina Paulo na Barnaba, wakawafukuza, watoke mipakani kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Wayuda wakawashawishi wakubwa wa muji pamoja na wanawake wamoja wenye heshima, walioabudu Mungu. Wakawatesa Paulo na Barnaba hata wakawafukuza toka katika inchi yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.