Acts 13:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo, upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Bar-yesu ambaye alijisingizia kuwa nabii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar-Yesu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walisafiri wakitisha kisiwa chote mpaka kwenye mji wa Pafo. Huko walimkuta mwanaume wa Kiyahudi aliyeitwa Bar-Yesu aliyekuwa akifanya uchawi. Alikuwa nabii wa uongo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Baryesu ambaye alijisingizia kuwa nabii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo, upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Bar-yesu ambaye alijisingizia kuwa nabii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar-Yesu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo, upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Bar-yesu ambaye alijisingizia kuwa nabii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakakikata kisiwa chote wakienda kwa miguu mpaka Pafo, hapo wakaona mtu wa Kiyuda aliyekuwa mganga na mwaguaji wa uwongo, jina lake Baryesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokwisha kupita katika kisanga chote, wakafika katika muji Pafo. Kule wakakutana na Muyuda mumoja aliyekuwa muchawi na nabii wa uongo, jina lake Bara-Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote cha Kupro, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa nwongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu: