Acts 13:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambaye alikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Paulo aliwaita Barnaba na Saulo ili asikie neno la Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa. Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikaa daima karibu na Sergio Paulo, aliyekuwa gavana na mtu makini sana. Sergio Paulo aliwaalika Barnaba na Sauli waende kumtembelea kwa sababu alitaka kusikia ujumbe wa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambaye alikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Paulo aliwaita Barnaba na Saulo ili asikie neno la Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambaye alikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Paulo aliwaita Barnaba na Saulo ili asikie neno la Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa, Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa. Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mtu huyu alikuwa pamoja na mtawala Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye mtawala akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambaye alikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Paulo aliwaita Barnaba na Saulo ili asikie neno la Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyo alikaa kwa mtawala nchi Sergio Paulo aliyekuwa mtu mwelekevu. Alipomwita Barnaba na Sauli kwa kutaka kulisikia Neno la Mungu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo alitumika pamoja na liwali mumoja mwenye akili, aliyeitwa Sergio Paulo. Liwali huyo akawaita Barnaba na Saulo wafike kwake kwa sababu alitaka kusikia Neno la Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paolo, mtu mwenye akili. Yeye akawaita Barnaba na Saul waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.