Acts 14:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, walianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katika sura za binadamu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umati ule wa watu walipoona yaliyokuwa yamefanywa na Paulo, wakapaza sauti, wakasema kwa lugha yao ya Kilikaonia, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu walipoona alichofanya Paulo, walipaza sauti kwa lugha yao wenyewe ya Kilikaonia. Walisema, “Miungu wamekuja kwetu katika maumbo ya kibinadamu!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, ulianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katika sura za binadamu!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, walianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katika sura za binadamu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ule umati wa watu ulipoona yale yaliyokuwa yamefanywa na Paulo, wakapiga kelele kwa lugha yao ya Kilikaonia wakasema, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ule umati wa watu ulipoona yaliyokuwa yamefanywa na Paulo, wakapiga kelele kwa lugha yao ya Kilikaonia wakasema, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa lugha ya Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, walianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katika sura za binadamu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makundi ya watu walipoona, Paulo alilolifanya, wakapaza sauti wakisema kwa Kilikaonia: Miungu imegeuka kufanana na sisi watu, ikatushukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati makundi ya watu walipoona jambo lile Paulo alilofanya, wakasema kwa sauti katika luga yao ya kilikaonia: “Miungu imetushukia ikiwa na sura ya kimutu!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na makutano walipoona aliyoyafanya Paolo wakapaaza sauti zao, wakisema kwa Kilukaonia, Mungu wametushukia kwa mifano ya wana Adamu.