Acts 14:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye kuhani wa hekalu la Zeu lililokuwa nje ya mji akaleta fahali na shada za maua mbele ya mlango mkuu wa mji, naye pamoja na ule umati wa watu akataka kuwatambikia mitume.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje kidogo tu ya mji, akaleta mafahali na mashada ya maua penye lango la mji kwa sababu yeye na umati ule wa watu walitaka kuwatolea dhabihu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng'ombe na taji za maua hata malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hekalu la Zeusi lilikuwa karibu na mji. Kuhani wa hekalu hili alileta mafahari ya ng'ombe kadhaa na mashada ya maua kwenye lango la mji. Kuhani na watu walitaka kuwatolea sadaka Paulo na Barnaba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye kuhani wa hekalu la Zeu lililokuwa nje ya mji akaleta fahali na shada za maua mbele ya mlango mkuu wa mji, na pamoja na ule umati wa watu akataka kuwatambikia mitume.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye kuhani wa hekalu la Zeu lililokuwa nje ya mji akaleta fahali na shada za maua mbele ya mlango mkuu wa mji, naye pamoja na ule umati wa watu akataka kuwatambikia mitume.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje kidogo tu ya mji, akaleta mafahali na mashada ya maua penye lango la mji kwa sababu yeye pamoja na ule umati wa watu walitaka kuwatolea dhabihu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje kidogo tu ya mji, akaleta mafahali na mashada ya maua penye lango la mji kwa sababu yeye na ule umati wa watu walitaka kuwatolea dhabihu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng'ombe na mataji ya maua hadi malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na umati wa watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye kuhani wa hekalu la Zeu lililokuwa nje ya mji akaleta fahali na shada za maua mbele ya mlango mkuu wa mji, naye pamoja na ule umati wa watu akataka kuwatambikia mitume.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mtambikaji wa nyumba ya Zeu iliyokuwa nje ya mji akaleta ng'ombe na vilemba vya maua malangoni, yeye na makundi ya watu wakataka kuwachinjia ng'ombe za tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng’ombe na taji za maua hata malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye kuhani wa hekalu la mungu Zeu, lililokuwa kwenye kiingilio cha muji, akaleta ngombe waliopambwa na mafungu za maua mbele ya mulango. Maana yeye pamoja na kundi la watu walitaka kuwatolea wale mitume sadaka ya nyama wenye kuchinjwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kuhani wa Zeu ambae hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ngʼombe na taji za maua hatta malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano.