Acts 14:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama nyinyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea Habari Njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa, mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Ndugu, kwa nini mnafanya hivi? Sisi si miungu. Ni wanadamu kama ninyi. Tulikuja kuwaambia Habari Njema. Tunawaambia mviache vitu hivi visivyo na thamani. Mgeukieni Mungu wa kweli aishiye, aliyeumba mbingu, nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama ninyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama nyinyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea habari njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na kila kitu kilicho ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea habari njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa, mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; tunawahubiria Habari Njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama nyinyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakisema: Waume, haya mnayafanyia nini? Hata sisi tu watu wenye kufa kama ninyi. Tunawapigia mbiu njema, mwiache miungu hii ya bure, mmgeukie Mungu Mwenye uzima aliyeziumba mbingu na nchi na bahari navyo vyote vilivyomo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Wandugu, kwa sababu gani munafanya mambo kama haya? Sisi vilevile ni watu, tuko sawasawa nanyi, na tunawahubiri ninyi Habari Njema kwamba muache kuabudu vitu hivi vya bure na mumugeukie Mungu mwenye uzima; yeye aliyeumba mbingu na dunia, bahari na vyote vinavyokuwa ndani yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sisi nasi tu wana Adamu hali moja na ninyi; twawakhubiri khabari njema mgenke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hayi, aliyeumba mbingu na inchi na bahari na vitu vyotc vilivyomo: