Acts 14:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: Huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hakuacha kuwaonesha watu uwepo wake: Ameonesha wema kwa kuwanyeshea mvua toka mbinguni na kuwapa mazao kwa majira yake, naye amewapa chakula tele na kuijaza mioyo yenu na furaha.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini daima Mungu alikuwepo na alitenda mambo mema yanayothibitisha kuwa yeye ni wa hakika na wa kweli. Huwapa mvua kutoka mbinguni na mavuno bora kwa wakati sahihi. Huwapa chakula tele na kuijaza mioyo yenu kwa furaha.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hakuacha kuwaonyesha watu uwepo wake: Ameonyesha wema kwa kuwanyeshea mvua toka mbinguni na kuwapa mazao kwa majira yake, naye amewapatia chakula tele na kuijaza mioyo yenu na furaha.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hakuacha kuwaonyesha watu uwepo wake: Ameonyesha wema kwa kuwanyeshea mvua toka mbinguni na kuwapa mazao kwa majira yake, naye amewapa chakula tele na kuijaza mioyo yenu na furaha.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: Huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini hakujitowesha kwenu, maana alifanya mema akiwapa mvua toka mbinguni na miaka ya mavuno mazuri, hivyo aliishibisha mioyo yenu vyakula na mashangilio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa vile hakuacha kujijulisha kwa njia ya kutenda mema. Anawanyeshea mvua toka mbingu, anawapa mavuno kwa wakati wake, anawapa chakula na kuwajaza na furaha.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Illakini hakujiacha hana shahidi kwa kuwa alitenda mema akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwajaza mioyo yenu chakula na furaha.