Acts 14:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, kisha, kwa kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kundi la waumini wa Isa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana Isa waliyemwamini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waliwachagua pia wazee katika kila kanisa na kuacha kula kwa muda ili kuwaombea. Wazee hawa walikuwa wanaume wanaomtumaini Bwana Yesu, hivyo Paulo na Barnaba wakamwomba Bwana awalinde.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, na baada ya kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, kisha, kwa kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kanisa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kundi la waumini, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana Isa waliyemwamini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, kisha, kwa kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila mahali penye wateule wakawawekea wazee, wakawapeleka kwa Bwana, ambaye walianza kumtegemea, wakiwaombea pamoja na kufunga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakawachagua wazee katika kila kanisa. Na kisha kuomba na kufunga kula chakula, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana waliyemwamini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini.