Acts 14:26 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudi Antiokia ambako hapo awali walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi wa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameitimiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka Atalia wakasafiri baharini wakarudi Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile huduma waliyokuwa wameikamilisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kutoka huko wakatweka tanga kwenda katika mji wa Antiokia ya Shamu. Huu ni mji ambako waamini waliwaweka katika uangalizi wa Mungu na kuwatuma kufanya kazi hii. Na sasa walikuwa wameimaliza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudi Antiokia ambako hapo awali walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi wa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameitimiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudi Antiokia ambako hapo awali walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi wa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameitimiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka huko Atalia wakasafiri baharini kwa merikebu wakarudi mpaka Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile kazi waliokuwa wamekamilisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka Atalia wakasafiri baharini wakarudi Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile huduma waliyokuwa wameikamilisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kutoka huko wakakabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudi Antiokia ambako hapo awali walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi wa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameitimiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko wakajipakia chomboni kwenda Antiokia; ndiko, walikotoka kwa kutumwa, wenzao wakiwaombea, Mungu awaongoze kwa upole katika kazi ile, waliyokwisha kuitimiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kutoka kule wakarudi mpaka Antiokia kwa njia ya chombo. Ni kule walipokuwa wameombewa neema kwa Mungu kwa ajili ya kazi ile waliyotoka kutimiza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kutoka huko wakasafiri baharini kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.