Acts 14:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa na mtu mmoja huko Lustra ambaye alikuwa kiwete tangu kuzaliwa, na alikuwa hajapata kutembea kamwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mji wa Listra, kulikuwa na kiwete, aliyekuwa amelemaa tangu kuzaliwa, na hakuwa ametembea kamwe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamaye, ambaye hajaenda kabisa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika mji wa Listra kulikuwa mtu aliyekuwa na tatizo katika mguu wake. Alizaliwa akiwa mlemavu wa miguu na hakuwahi kutembea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulikuwa na mtu mmoja huko Lustra ambaye alikuwa amelemaa miguu tangu kuzaliwa, na alikuwa hajapata kutembea kamwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa na mtu mmoja huko Lustra ambaye alikuwa kiwete tangu kuzaliwa, na alikuwa hajapata kutembea kamwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mji wa Listra, alikuweko kiwete, ambaye alikuwa amelemaa tangu kuzaliwa na hakuwa ametembea kamwe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mji wa Listra, alikuwako kiwete, ambaye alikuwa amelemaa tangu kuzaliwa na hakuwa ametembea kamwe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, asiyeweza kutumia miguu yake na aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa na mtu mmoja huko Lustra ambaye alikuwa kiwete tangu kuzaliwa, na alikuwa hajapata kutembea kamwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Listira kulikuwa na mtu aliyekaa hawezi miguu; ni kiwete tangu hapo, alipotoka tumboni mwa mama yake, hakuweza kwenda kamwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamaye, ambaye hajaenda kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kule Listra kulikuwa mutu mumoja aliyekuwa kiwete tangia kuzaliwa. Yeye hakuweza kusimama wala kupima kutembea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na huko Lustra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mama yake, ambae hajaenda kabisa.