Acts 15:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeo kama alivyoamuru Mose, hamtaweza kuokolewa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Yudea, nao wakawa wanawafundisha waumini: “Msipotahiriwa kulingana na desturi aliyofundisha Musa, hamwezi kuokoka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha baadhi ya watu kutoka Uyahudi wakaja Antiokia na kuanza kuwafundisha jamii ya waamini wasio Wayahudi, wakisema, “Hamwezi kuokolewa ikiwa hamkutahiriwa kama Musa alivyotufundisha.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeo ya Sheria ya Mose, hamtaweza kuokolewa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeo kama alivyoamuru Mose, hamtaweza kuokolewa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Uyahudi, nao wakawa wanawafundisha ndugu walioamini kwamba, “Isipokuwa mmetahiriwa kufuatana na desturi aliyofundisha Mose, hamwezi kuokoka.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Uyahudi, nao wakawa wanawafundisha wandugu: “Msipotahiriwa kufuatana na desturi aliyofundisha Musa, hamwezi kuokoka.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakashuka watu waliotoka Yudea wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamuwezi kuokoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeo kama alivyoamuru Mose, hamtaweza kuokolewa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulikuwa na watu waliotelemka toka Yudea, wakaja huko, wakawafundisha ndugu kwamba: Hamwezi kuokoka msipotahiriwa, kama Mose alivyotuzoeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wamoja walishuka toka Yudea kwenda Antiokia, nao wakaanza kuwafundisha wandugu waamini kwamba hawawezi kuokoka ikiwa hawatahiriwi sawa vile inavyoagizwa katika Sheria ya Musa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
WAKASHUKA wafu waliotoka Yahudi wakawafundisha ndugu ya kama, Msipotahiriwa na kuifuata desturi ya Musa hamwezi kuokoka.