Acts 15:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa basi, kwa nini kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hao waumini mzigo ambao wala babu zetu, wala sisi hatukuweza kuubeba?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuweka nira shingoni mwa wanafunzi ambayo baba zetu wala sisi hatukuweza kuibeba?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa nini sasa mnawatwisha mzigo mzito kwenye shingo zao? Je, mnajaribu kumkasirisha Mungu? Sisi na baba zetu hatukuweza kuubeba mzigo huo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa basi, kwa nini kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hao waumini mzigo ambao wala babu zetu, wala sisi hatukuweza kuubeba?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa basi, kwa nini kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hao waumini mzigo ambao wala babu zetu, wala sisi hatukuweza kuubeba?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuweka kongwa shingoni mwa wanafunzi ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulibeba?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuweka kongwa shingoni mwa wanafunzi ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulibeba?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulibeba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa basi, kwa nini kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hao waumini mzigo ambao wala babu zetu, wala sisi hatukuweza kuubeba?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa mwamjaribiaje Mungu mkiwatwisha wanafunzi mzigo, ambao baba zetu hawakuweza kuuchukua, uliotushinda nasi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi sasa, kwa nini munataka kumupima Mungu kwa kuwabebesha muzigo ambao wala babu zetu, wala sisi wenyewe hatukuweza kuubeba?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka nira juu ya shingo za wanafunzi, ambayo baba zetu na sisi hatukuweza kuichukua.