Acts 15:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kikundi chote kilikaa kimya, kikawasikiliza Barnaba na Paulo wakieleza miujiza na maajabu ambayo Mungu alitenda kwa mikono yao kati ya watu wa mataifa mengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kusanyiko lote wakakaa kimya, wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu wa Mataifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo kundi lote likawa kimya. Waliwasikiliza Paulo na Barnaba walipokuwa wanaeleza kuhusu ishara na maajabu ambayo kupitia wao Mungu aliwatendea watu wasio Wayahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kikundi chote kilikaa kimya, kikawasikiliza Barnaba na Paulo wakieleza miujiza na maajabu ambayo Mungu alitenda kwa mikono yao kati ya watu wa mataifa mengine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kikundi chote kilikaa kimya, kikawasikiliza Barnaba na Paulo wakieleza miujiza na maajabu ambayo Mungu alitenda kwa mikono yao kati ya watu wa mataifa mengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kusanyiko lote likakaa kimya, wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu Mataifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kusanyiko lote likakaa kimya, wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu wa Mataifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kikundi chote kilikaa kimya, kikawasikiliza Barnaba na Paulo wakieleza miujiza na maajabu ambayo Mungu alitenda kwa mikono yao kati ya watu wa mataifa mengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, mkutano wote ukanyamaza, wakamsikiliza Barnaba na Paulo, wakivisimulia vielekezo na vioja vyote, Mungu alivyovifanya kwa mikono yao katika wamizimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mukutano wote ukabaki kimya ukisikiliza maelezo ya Barnaba na Paulo juu ya vitambulisho na maajabu yote Mungu aliyofanya kwa njia yao katikati ya watu wa mataifa mengine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paolo wakiwapasha khabari za ishara na maajabu ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika mataifa.