Acts 15:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jambo hili lilisababisha ubishi mkubwa, na baada ya Paulo na Barnaba kujadiliana nao, ikaamuliwa Paulo na Barnaba pamoja na waumini kadhaa wa lile kanisa la Antiokia waende Yerusalemu kuwaona wale mitume na wazee kuhusu jambo hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Paulo na Barnaba kutokubaliana nao kukawa na mabishano makali, Paulo na Barnaba na baadhi ya wengine miongoni mwao wakachaguliwa kwenda Yerusalemu ili kujadiliana jambo hili na mitume na wazee.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo na Barnaba wakayapinga mafundisho haya na wakahojiana na kubishana na watu hawa juu ya hili. Hivyo kundi la waamini likaamua kuwatuma Paulo, Barnaba, na baadhi ya watu wengine Yerusalemu ili kujadiliana na mitume na wazee kuhusu suala hili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jambo hili lilisababisha ubishi mkubwa, na baada ya Paulo na Barnaba kujadiliana nao, ikaamuliwa Paulo na Barnaba pamoja na waumini kadhaa wa lile kanisa la Antiokia waende Yerusalemu kuwaona wale mitume na wazee kuhusu jambo hilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jambo hili lilisababisha ubishi mkubwa, na baada ya Paulo na Barnaba kujadiliana nao, ikaamuliwa Paulo na Barnaba pamoja na waumini kadhaa wa lile kanisa la Antiokia waende Yerusalemu kuwaona wale mitume na wazee kuhusu jambo hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Paulo na Barnaba kutokukubaliana nao kukawa na mabishano makali, Paulo na Barnaba na baadhi ya wengine miongoni mwao wakachaguliwa kuingia Yerusalemu ili kujadiliana jambo hili na mitume na wazee.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Paulo na Barnaba kutokubaliana nao kukawa na mabishano makali, Paulo na Barnaba na baadhi ya wengine miongoni mwao wakachaguliwa kwenda Yerusalemu ili kujadiliana jambo hili na mitume na wazee.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee ili kuzungumza juu ya suala hilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jambo hili lilisababisha ubishi mkubwa, na baada ya Paulo na Barnaba kujadiliana nao, ikaamuliwa Paulo na Barnaba pamoja na waumini kadhaa wa lile kanisa la Antiokia waende Yerusalemu kuwaona wale mitume na wazee kuhusu jambo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Paulo na Barnaba wakabishana nao kabisa na kushindana sana. Kisha wakamwagiza Paulo na Barnaba na wenzao wengine, wapande kwenda Yerusalemu kwao mitume na wazee kwa ajili ya mshindano huu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Paulo na Barnaba wakapingana na kubishana nao vikali sana juu ya jambo hili. Na kwa hiyo wandugu waamini wakaagiza Paulo na Barnaba pamoja na watu wengine kati yao waende Yerusalema kusemezana na mitume na wazee wa kanisa la kule juu ya maneno yale.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo.