Acts 15:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakawapa barua hii: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimuni nyinyi ndugu wa mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakatumwa na barua ifuatayo: Sisi mitume na wazee, ndugu zenu. Kwa waumini wa Mataifa mlio Antiokia, Siria na Kilikia. Salamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kundi la waamini likaandika barua na kuwatuma watu hawa. Barua ilisema: Kutoka kwa mitume na wazee, ndugu zenu. Kwa ndugu wote wasio Wayahudi katika mji wa Antiokia na katika majimbo ya Shamu na Kilikia. Ndugu Wapendwa:
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakawapa barua hii: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimuni ninyi ndugu wa mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakawapa barua hii: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimuni nyinyi ndugu wa mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakatumwa na barua ifuatayo: Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, Kwa ndugu Mataifa mlioamini mlioko Antiokia, Shamu na Kilikia: Salamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakatumwa na barua ifuatayo: Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, Kwa ndugu Mataifa mlioamini mlioko Antiokia, Shamu na Kilikia: Salamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakawapa barua hii: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimuni nyinyi ndugu wa mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaandika barua, waipeleke mikononi mwao, ni ya kwamba: Sisi mitume na wazee tunawaamkia kindugu ninyi ndugu zetu huko Antiokia na Ushami na Kilikia mliotoka kwa wamizimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakawatuma na barua iliyoandikwa hivi: “Sisi mitume na wazee wa kanisa na wandugu zenu, tunawasalimu ninyi wandugu zetu waamini wa mataifa mengine munaokuwa katika muji wa Antiokia na katika jimbo la Suria na la Kilikia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.