Acts 15:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msile vyakula vilivyotambikiwa vinyago; msinywe damu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwamba mjiepushe na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na mjiepushe na uasherati. Mkiyaepuka mambo haya, mtakuwa mmefanya vyema. Kwaherini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Msile chakula kilichotolewa kwa sanamu. Msile nyama inayotokana na wanyama walionyongwa au nyama ambayo bado ina damu ndani yake. Msijihusishe na uzinzi. Mkijitenga na mambo haya, mtakuwa mnaenenda vyema. Wasalamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msile vyakula vilivyotambikiwa sanamu; msinywe damu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msile vyakula vilivyotambikiwa vinyago; msinywe damu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwamba mjiepushe na kitu cho chote kilichotolewa sadaka kwa sanamu, kunywa damu, nyama ya wanyama walionyongwa na mjiepushe na uasherati. Mkiyaepuka mambo haya mtakuwa mmefanya vyema. Kwaherini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwamba mjiepushe na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na mjiepushe na uasherati. Mkiyaepuka mambo haya, mtakuwa mmefanya vyema. Kwaherini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msile vyakula vilivyotambikiwa vinyago; msinywe damu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mshike mzio wa nyama za tambiko na wa damu na wa nyamafu na wa ugoni. Mkijikataza mambo haya mtafanya vema. Kaeni vema! Salamu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
musikule vyakula vilivyotolewa kwa kutambikia sanamu; musikule damu wala nyamafu; na muepuke uasherati. Mutafanya vema kama mukijitenga na mambo haya. Salamu kwenu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongwa, na asharati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Salamu.