Acts 15:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wakatumwa na waumini. Wakapitia Foinike na Samaria, wakielezea jinsi watu wa Mataifa walivyoongoka. Habari hizi zikaleta furaha kubwa kwa ndugu wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kanisa liliwapa wale waliotumwa kila kitu walichohitaji kwa ajili ya safari yao. Walisafiri kupitia maeneo ya Foeniki na Samaria, ambako walieleza kwa undani mambo yote namna ambavyo wasio Wayahudi wamemgeukia Mungu wa kweli. Habari hii iliwafurahisha waamini wote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wakasafirishwa na kanisa, wakiwa njiani wakapitia Samaria wakawaeleza jinsi watu Mataifa walivyoongoka. Habari hizi zikaleta furaha kubwa kwa ndugu wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wakasafirishwa na waumini. Wakiwa njiani wakapitia nchi ya Foinike na Samaria, wakawaeleza jinsi watu wa Mataifa walivyookoka. Habari hizi zikaleta furaha kubwa kwa ndugu wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakasindikizwa na wateule, wakapita Ufoniki na Samaria, wakaeleza Po pote, wamizimu walivyogeuka; hivyo wakawafurahisha sana ndugu wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kanisa liliwapatia vitu walivyohitaji kwa ajili ya safari ile, nao wakapita katika inchi ya Foinikia na katika Samaria. Na kule wakaeleza namna watu wa mataifa mengine walivyomugeukia Mungu. Habari hii ikafurahisha sana wandugu waamini wote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, wakisafirishwa na Kanisa, wakapita kati ya inchi ya Foiniki na Samaria, wakitangaza khabari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.