Acts 15:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kuwaaga, hao wajumbe walielekea Antiokia ambako waliita mkutano wa waumini, wakawapa hiyo barua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wakaagwa, wakashuka kwenda Antiokia. Baada ya kulikusanya kundi la waumini pamoja, wakawapa ile barua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata hao wakiisha kupewa ruhusa wakatelemkia Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ile barua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo Paulo, Barnaba, Yuda, na Sila waliondoka Yerusalemu na kwenda Antiokia. Walipofika huko walilikusanya kundi la waamini pamoja na wakawapa barua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya kuwaaga, hao wajumbe walielekea Antiokia ambako waliita mkutano wa waumini, wakawapa hiyo barua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kuwaaga, hao wajumbe walielekea Antiokia ambako waliita mkutano wa waumini, wakawapa hiyo barua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wakaagwa, wakashuka kwenda Antiokia. Baada ya kulikusanya kanisa pamoja, wakawapa ile barua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wakaagwa, wakashuka kwenda Antiokia. Baada ya kulikusanya kundi lote la waumini pamoja, wakawapa ile barua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata hao wakiisha kupewa ruhusa wakateremka kwenda Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ile barua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kuwaaga, hao wajumbe walielekea Antiokia ambako waliita mkutano wa waumini, wakawapa hiyo barua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakasindikizwa, wakatelemka kwenda Antiokia, wakawakusanya wao wote wa hilo kundi, wakawatolea ile barua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata hao wakiisha kupewa ruhusa wakatelemkia Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ile barua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kuagana, wale wajumbe wakaondoka na kwenda Antiokia. Kule wakakusanya kundi lote la waamini, wakawapa barua ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta hao wakiisha kupewa rukhusa wakatelemkia Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ule waraka.