Acts 15:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo walisimama, wakasema, “Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na kufundishwa kuifuata sheria.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo baadhi ya waumini waliokuwa wa dhehebu la Mafarisayo wakasimama na kusema, “Hao watu wa Mataifa lazima watahiriwe na waagizwe kutii Torati ya Musa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya waamini mjini Yerusalemu waliokuwa Mafarisayo, walisimama na kusema, “Waamini wasio Wayahudi lazima watahiriwe. Ni lazima tuwaambie waitii Sheria ya Musa!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo walisimama, wakasema, “Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na kufundishwa kuifuata Sheria ya Mose.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo walisimama, wakasema, “Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na kufundishwa kuifuata sheria.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo baadhi ya walioamini wa madhehebu ya Mafarisayo wakasimama na kusema, “Hao watu Mataifa lazima watahiriwe na waagizwe kuzitii sheria za Mose.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo baadhi ya walioamini wa madhehebu ya Mafarisayo wakasimama na kusema, “Hao watu wa Mataifa lazima watahiriwe na waagizwe kutii Torati ya Musa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo walisimama, wakasema, “Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na kufundishwa kuifuata sheria.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pakainuka waliokuwa wa chama cha Mafariseo, lakini nao walikuwa wenye kumtegemea Bwana, wakasema: Sharti watahiriwe! Sharti waagizwe kuyashika Maonyo ya Mose!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wanafunzi wamoja waliokuwa katika chama cha Wafarisayo wakasimama na kusema: “Sherti watu wa mataifa mengine walioamini watahiriwe na kuagizwa wafuate Sheria ya Musa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.