Acts 15:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Mungu anayejua mioyo ya watu, alithibitisha kwamba amewakubali kwa kuwapa nao Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu, ajuaye mioyo ya watu, alionesha kwamba anawakubali kwa kuwapa Roho Mtakatifu wa Mungu kama vile alivyotupatia sisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu anamfahamu kila mtu, hata mawazo yao, na amewakubali watu hawa wasio Wayahudi. Amelionyesha hili kwetu kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Mungu anayejua mioyo ya watu, alithibitisha kwamba amewakubali kwa kuwapa nao Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Mungu anayejua mioyo ya watu, alithibitisha kwamba amewakubali kwa kuwapa nao Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu, yeye ajuaye mioyo, alionyesha kwamba anawakubali kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama vile alivyotupa sisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu, yeye ajuaye mioyo, alionyesha kwamba anawakubali kwa kuwapa Roho wa Mwenyezi Mungu kama vile alivyotupa sisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Mungu anayejua mioyo ya watu, alithibitisha kwamba amewakubali kwa kuwapa nao Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Mungu mwenye kuitambua mioyo akawapokea wamizimu alipowapa Roho Mtakatifu, kama alivyotupa na sisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Mungu anayejua mafikiri ya mutu, alihakikisha kwamba amewakubali watu wa mataifa mengine kwa njia ya kuwapatia Roho Mutakatifu sawa vile alivyotupatia sisi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Mungu, ajuae mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vilevile kama alivyotupa sisi;