Acts 16:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara baada ya Paulo kuona maono hayo, tulijitayarisha kwenda Makedonia bila kukawia, tukiwa na hakika kwamba Mungu ametuita tuwahubirie Habari Njema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Paulo kuona maono haya, tulijiandaa kwa haraka kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kuwa Mungu alikuwa ametuita kuhubiri Injili huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya Paulo kuona maono yale, tulijiandaa haraka na tukaondoka kwenda Makedonia. Tulielewa kuwa Mungu ametuita ili tukahubiri Habari Njema huko Makedonia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mara baada ya Paulo kuona ono hilo, tulijitayarisha kwenda Makedonia bila kukawia, tukiwa na hakika kwamba Mungu ametuita tuwapelekee Habari Njema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara baada ya Paulo kuona maono hayo, tulijitayarisha kwenda Makedonia bila kukawia, tukiwa na hakika kwamba Mungu ametuita tuwahubirie Habari Njema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Paulo kuona maono haya, mara tulijiandaa kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kwa hakika kwamba Mungu ametuita kuhubiri habari njema huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Paulo kuona maono haya, tulijiandaa kwa haraka kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kuwa Mungu alikuwa ametuita kuhubiri habari njema huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubirie Habari Njema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara baada ya Paulo kuona maono hayo, tulijitayarisha kwenda Makedonia bila kukawia, tukiwa na hakika kwamba Mungu ametuita tuwahubirie Habari Njema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kuiona njozi hiyo, papo hapo tukatafuta, jinsi tutakavyovuka, tuje Makedonia, maana sote tumejua kweli, ya kuwa ni Mungu aliyetuita, tuje, tuwapigie hiyo mbiu njema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na pale pale kisha kupata maono yale, tukajitayarisha kwenda Makedonia, kwa maana tulitambua hakika kwamba Mungu alituita kwenda kuhubiri Habari Njema kule.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi alipokwisha kuona yale maono, marra tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Bwana ametuita tuwakhubiri Injili.