Acts 16:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka huko tukasafiri hadi Filipi, mji mkuu wa jimbo hilo la Makedonia, uliokuwa koloni ya Warumi. Nasi tukakaa huko siku kadhaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha tulisafiri kwa nchi kavu mpaka Filipi, koloni la Rumi na mji maarufu katika la Makedonia. Tulikaa pale kwa siku chache.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka huko tukasafiri hadi Filipi, mji mkuu wa Makedonia sehemu walipokuwa wanakaa Warumi, nasi tukakaa kwenye mji huo kwa siku kadhaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka huko tukasafiri hadi Filipi, mji mkuu wa jimbo hilo la Makedonia, uliokuwa koloni ya Warumi. Nasi tukakaa huko siku kadhaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukakaa siku kadhaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Toka huko tukafika Filipi, ni mji wa mbele wa upande huo wa Makedonia, tena ndimo, Waroma walimotua. Tulipokuwa tumekaa mjini mle siku kidogo
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutoka kule tukafika mpaka Filipi, muji mukubwa wa inchi ya Makedonia uliokuwa chini ya utawala wa Waroma. Nasi tukakaa katika muji ule kwa muda wa siku chache.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Siku ya pili tukafika Neapoli na kutoka hapo tukafika Filippi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika wilaya ile, nayo ni Kolonia ya Kirumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.