Acts 16:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya Sabato tukaenda nje ya lango la mji kando ya mto, ambapo tulitarajia kupata mahali pa kufanyia maombi. Tukaketi, tukaanza kuongea na baadhi ya wanawake waliokuwa wamekusanyika huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku ya Sabato tulikwenda mtoni, nje ya lango la mji. Tulidhani tungepata mahali ambapo Wayahudi hukutana mara kwa mara kwa ajili ya kuomba. Baadhi ya wanawake walikuwa wamekusanyika huko, na hivyo tulikaa chini na kuzungumza nao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya Sabato tukaenda nje ya lango la mji kando ya mto, mahali ambapo tulitarajia tungepata mahali pa kufanyia maombi. Tukaketi, tukaanza kuongea na baadhi ya wanawake waliokuwa wamekusanyika huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya Sabato tukaenda nje ya lango la mji kando ya mto, mahali ambapo tulitarajia tungepata mahali pa kufanyia maombi. Tukaketi, tukaanza kuongea na baadhi ya wanawake waliokuwa wamekusanyika huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
tukatoka langoni kwenda nje siku ya mapumziko, tukaenda kando ya mto, tulipowazia kuwa pao pa kuombea. Ndipo, tulipokaa, tukisema na wanawake waliokusanyika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya Sabato ilipotimia tukatoka ndani ya muji ule na kwenda karibu na muto mumoja, kwenye nafasi tulipozania kuwa ya kufanyia maombi. Tukaikaa na kusemezana na wanawake waliokusanyika pale.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, tukidhani ya kuwa hapo pana mahali pii kuomba; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.