Acts 16:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miongoni mwa wale waliotusikiliza alikuwa mwanamke mmoja mcha Mungu aitwaye Ludia mwenyeji wa Thuatira, ambaye alikuwa mfanyabiashara ya nguo za kitani za rangi ya zambarau. Bwana aliufungua moyo wake hata akayapokea yale maneno Paulo aliyokuwa anasema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mfanyabiashara wa nguo za zambarau, raia wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu. Mwenyezi Mungu akaufungua moyo wake akaupokea ujumbe wa Paulo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Miongoni mwao alikuwepo mwanamke aliyeitwa Lydia kutoka katika mji wa Thiatira. Alikuwa mwuza rangi ya zambarau. Alikuwa mwabudu Mungu wa kweli. Lydia alimsikiliza Paulo, na Bwana akaufungua moyo wake kuyakubali yale Paulo alikuwa anasema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Miongoni mwa wale waliotusikiliza alikuwa mwanamke mmoja mcha Mungu aitwaye Ludia mwenyeji wa Thuatira, ambaye alikuwa mfanyabiashara ya nguo za kitani za rangi ya zambarau. Bwana aliufungua moyo wake hata akayapokea yale maneno Paulo aliyokuwa anasema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miongoni mwa wale waliotusikiliza alikuwa mwanamke mmoja mcha Mungu aitwaye Ludia mwenyeji wa Thuatira, ambaye alikuwa mfanyabiashara ya nguo za kitani za rangi ya zambarau. Bwana aliufungua moyo wake hata akayapokea yale maneno Paulo aliyokuwa anasema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mfanya biashara wa nguo za zambarau, mwenyeji wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu. Bwana akaufungua moyo wake akaupokea ujumbe wa Paulo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mfanyabiashara wa nguo za zambarau, mwenyeji wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu. Mwenyezi Mungu akaufungua moyo wake, akaupokea ujumbe wa Paulo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miongoni mwa wale waliotusikiliza alikuwa mwanamke mmoja mcha Mungu aitwaye Ludia mwenyeji wa Thuatira, ambaye alikuwa mfanyabiashara ya nguo za kitani za rangi ya zambarau. Bwana aliufungua moyo wake hata akayapokea yale maneno Paulo aliyokuwa anasema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Palikuwapo mwanamke, jina lake Lidia; alitoka mji wa Tiatira, akawa mchuuzi wa nguo za kifalme. Kwa sababu alimcha Mungu, akasikiliza. Naye Bwana akamfunulia moyo, ayashike yaliyosemwa na Paulo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kati ya wanawake wale kulikuwa mwanamuke mumoja aliyeitwa Ludia, wa muji Tuatera. Yeye alikuwa muchuuzi wa nguo nyekundu za bei kali na mwenye kuogopa Mungu. Mwanamuke yule akatusikiliza kwa maana Bwana alimufungua moyo kusudi apate kufuata kabisa maneno Paulo aliyosema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwanamke mnioja, jina lake Ludia, mwenye kuuza rangi ya zambarao, mwenyeji wa Thuatira, mcha Mungu, akatusikiliza. Moyo wake huyu ukafunguliwa na Bwana, ayaangalie mineno yaliyonenwa na Paolo.