Acts 16:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya huyo mama pamoja na jamaa yake kubatizwa, alitualika akisema, “Kama kweli mmeona kwamba mimi namwamini Bwana, karibuni nyumbani kwangu mkakae.” Akatuhimiza twende.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi alipokwisha kubatizwa yeye na watu wa nyumba yake, alitukaribisha nyumbani mwake, akisema, “Kama mmeona kweli mimi nimemwamini Bwana Isa, karibuni mkae nyumbani mwangu.” Naye akatushawishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatushurutisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yeye na watu wote waliokuwa wakiishi katika nyumba yake walibatizwa. Kisha akatualika nyumbani mwake. Alisema, “Ikiwa mnaona mimi ni mwamini wa kweli wa Bwana Yesu, njooni mkae nyumbani mwangu.” Alitushawishi tukae nyumbani mwake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya huyo mama pamoja na jamaa yake kubatizwa, alitualika akisema, “Kama kweli mmeona kwamba mimi namwamini Bwana, karibuni nyumbani kwangu mkakae.” Akatuhimiza twende.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya huyo mama pamoja na jamaa yake kubatizwa, alitualika akisema, “Kama kweli mmeona kwamba mimi namwamini Bwana, karibuni nyumbani kwangu mkakae.” Akatuhimiza twende.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi alipokwisha kubatizwa yeye na watu wa nyumbani mwake, alitukaribisha nyumbani mwake akisema, “Kama mmeona kweli mimi nimemwamini Bwana, karibuni mkae nyumbani mwangu.” Naye akatushawishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi alipokwisha kubatizwa yeye na watu wa nyumba yake, alitukaribisha nyumbani kwake akisema, “Kama mmeona kweli mimi nimemwamini Bwana Isa, karibuni mkae nyumbani mwangu.” Naye akatushawishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatusihi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya huyo mama pamoja na jamaa yake kubatizwa, alitualika akisema, “Kama kweli mmeona kwamba mimi namwamini Bwana, karibuni nyumbani kwangu mkakae.” Akatuhimiza twende.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kubatizwa pamoja nao waliokuwamo mwake akatubembeleza na kusema: Kama mmeniona mimi kwamba: Ni mwenye kumtegemea Bwana, mwingie mwangu, mkae! Ndivyo, alivyotushurutisha.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatushurutisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha yeye na watu wa nyumba yake wakabatizwa. Naye akatusihi akisema: “Ikiwa munakubali kweli kwamba ninamwamini Bwana, basi mufike mupange ndani ya nyumba yangu.” Akatulazimisha tuitike.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta alipokwisha kumbatiza, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae; akatushurutisha.