Acts 16:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawa anafanya hivyo kwa siku nyingi hata siku moja Paulo alikasirika, akamgeukia na kumwambia huyo pepo, “Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu!” Mara huyo pepo akamtoka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaendelea kufanya hivi kwa siku nyingi, lakini Paulo akiwa ameudhika sana, akageuka na kumwambia yule pepo mchafu, “Ninakuamuru katika jina la Isa Al-Masihi, umtoke!” Yule pepo mchafu akamtoka mara hiyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliendelea kufanya hivi kwa siku kadhaa na ikamuudhi Paulo, akageuka na kumkemea yule roho akisema, “Kwa uwezo wa Yesu Kristo, ninakuamuru utoke ndani yake!” Mara ile roho chafu ikamtoka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akawa anafanya hivyo kwa siku nyingi hata siku moja Paulo alikasirika, akamgeukia na kumwambia huyo pepo, “Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu!” Mara huyo pepo akamtoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawa anafanya hivyo kwa siku nyingi hata siku moja Paulo alikasirika, akamgeukia na kumwambia huyo pepo, “Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu!” Mara huyo pepo akamtoka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaendelea kufanya hivi kwa siku nyingi, lakini Paulo akiwa ameudhika sana, akageuka na kumwambia yule pepo mchafu, “Ninakuamuru katika jina la Yesu Kristo, umtoke!” Yule pepo mchafu akamtoka saa ile ile.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaendelea kufanya hivi kwa siku nyingi, lakini Paulo akiwa ameudhika sana, akageuka na kumwambia yule pepo mchafu, “Ninakuamuru katika jina la Isa Al-Masihi, umtoke!” Yule pepo mchafu akamtoka saa ile ile.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawa anafanya hivyo kwa siku nyingi hata siku moja Paulo alikasirika, akamgeukia na kumwambia huyo pepo, “Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu!” Mara huyo pepo akamtoka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipovifanya siku nyingi, vikamwumiza Paulo, akageuka, akamwambia yule pepo: Nakuagiza wewe kwa Jina la Yesu Kristo, umtoke! Naye akamtoka saa ileile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akafanya hivi kwa muda wa siku nyingi. Na kwa mwisho Paulo akachukizwa naye. Basi akageuka na kumwambia yule pepo: “Ninakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, utoke ndani yake!” Na saa ile ile yule pepo akatoka ndani yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawa akifanya hayo siku nyingi. Lakini Paolo akakasirika akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.