Acts 16:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, “Watu hawa ni Wayahudi na wanafanya fujo katika mji wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kuwafikisha mbele ya mahakimu wakawashtaki wakisema, “Hawa watu wanaleta ghasia katika mji wetu, nao ni Wayahudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakawaleta Paulo na Sila mbele ya maofisa wa Kirumi na kusema, “Watu hawa ni Wayahudi, wanafanya vurugu katika mji wetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, “Watu hawa ni Wayahudi na wanafanya fujo katika mji wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, “Watu hawa ni Wayahudi na wanafanya fujo katika mji wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kuwafikisha mbele ya mahakimu wakawashtaki wakisema, “Hawa watu wanaleta ghasia katika mji wetu, nao ni Wayahudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kuwafikisha mbele ya mahakimu wakawashtaki wakisema, “Hawa watu wanaleta ghasia katika mji wetu, nao ni Wayahudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakawapeleka kwa mahakimu, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, “Watu hawa ni Wayahudi na wanafanya fujo katika mji wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakawapeleka kwa mabwana wakubwa, wakasema: Watu hawa wanauchafua mji wetu; ni Wayuda,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipowafikisha kwa watawala wa Waroma, wakasema: “Watu hawa ni Wayuda, nao wanaleta fujo katika muji wetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanataharakisha mji wetu, nao ni Wayahudi.