Acts 16:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kundi la watu likajiunga likawashambulia; na wale mahakimu wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakaamuru wapigwe viboko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umati wa watu wakajiunga kuwashambulia Paulo na Sila, na wale mahakimu wakaamuru wavuliwe nguo zao na wapigwe mijeledi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Umati wote wa watu ukawa kinyume na Paulo na Sila. Maofisa wakawachania nguo Paulo na Sila na wakaamuru wapigwe bakora.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kundi la watu likajiunga nao, likawashambulia. Wale mahakimu wakawatatulia Paulo na Sila mavazi yao, wakaamuru wapigwe viboko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kundi la watu likajiunga likawashambulia; na wale mahakimu wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakaamuru wapigwe viboko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Umati wa watu waliokuwepo wakajiunga katika kuwashambulia Paulo na Sila na wale mahakimu wakaamuru wavuliwe nguo zao na wachapwe viboko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Umati wa watu waliokuwepo wakajiunga katika kuwashambulia Paulo na Sila na wale mahakimu wakaamuru wavuliwe nguo zao na wachapwe viboko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Makutano wote wakaondoka wakawaendea, mahakimu wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kundi la watu likajiunga likawashambulia; na wale mahakimu wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakaamuru wapigwe viboko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wengi walipoinuka kuwaendea kwa nguvu, mabwana wakubwa wakawapokonya mavazi yao, wakaagiza, wapigwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kundi la watu waliokuwa pale wakawashambulia Paulo na Sila, nao watawala wakaamuru wawavue nguo kwa kinguvu na kuwapiga fimbo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Makutano wote wakaondoka wakawaendea, Makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.