Acts 16:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kuwapiga sana, wakawatupa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walichapwa sana kisha wakawekwa gerezani. Maofisa wakamwambia mkuu wa gereza, “Walinde watu hawa kwa umakini!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kuchapwa sana wakatupwa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kuwachapa sana, wakawatupa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha kuwapiga viboko vingi wakawatia kifungoni, wakamwagiza mlinda kifungo, awatie mahali pasipoingilikana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokwisha kuwapiga sana, wakawatia ndani ya kifungo na kumwagiza mulinzi wa kifungo awachunge kabisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.