Acts 16:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Paulo alitaka Timotheo aandamane naye safarini, kwa hiyo alimtahiri. Alifanya hivyo kwa sababu Wayahudi wote walioishi sehemu hizo walijua kwamba baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo alitaka Timotheo aandamane naye, hivyo akamtahiri kwa sababu ya Wayahudi walioishi eneo lile, kwa maana wote walimjua baba yake ni Myunani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo alitaka kusafiri pamoja na Timotheo, lakini Wayahudi wote walioishi katika eneo lile walijua kuwa baba yake alikuwa Myunani. Hivyo ikamlazimu Paulo amtahiri Timotheo ili kuwaridhisha Wayahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Paulo alitaka Timotheo aandamane naye safarini, kwa hiyo alimtahiri. Alifanya hivyo kwa sababu Wayahudi wote walioishi sehemu hizo walijua kwamba baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Paulo alitaka Timotheo aandamane naye safarini, kwa hiyo alimtahiri. Alifanya hivyo kwa sababu Wayahudi wote walioishi sehemu hizo walijua kwamba baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo alitaka Timotheo afuatane naye, hivyo akamchukua na kumtahiri kwa sababu ya Wayahudi waliokuwa wanaishi eneo lile kwa maana wote walimjua baba yake ni Myunani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo alitaka Timotheo afuatane naye, hivyo akamchukua na kumtahiri kwa sababu ya Wayahudi waliokuwa wanaishi eneo lile kwa maana wote walimjua baba yake ni Myunani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Mgiriki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Paulo alitaka Timotheo aandamane naye safarini, kwa hiyo alimtahiri. Alifanya hivyo kwa sababu Wayahudi wote walioishi sehemu hizo walijua kwamba baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Paulo alimtaka, aondoke kwenda naye. Akamchukua, akamtahiri kwa ajili ya Wayuda waliokuwa katika miji ile, kwani wote walimjua, ya kuwa baba yake alikuwa Mgriki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Paulo alitaka Timoteo amusindikize katika safari zake. Kwa hiyo akamutahiri kwa sababu ya Wayuda waliokaa katika pande zile, kwa maana wote walijua kwamba baba yake alikuwa Mugriki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Paolo akamtaka huyu afuatane nae, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile: kwa maana wote walijua ya kuwa baba yake ni Myunani.