Acts 16:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Paulo alimjibu, “Ati nini? Ingawa hatukuwa na kosa, walitupiga viboko hadharani hali sisi ni raia wa Roma. Tena, walitutia ndani na sasa wanataka kutufungulia kwa siri! Hata kidogo! Ni lazima wao wenyewe waje hapa watufungulie.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Paulo akawaambia wale maafisa, “Wametupiga hadharani bila kutufanyia mashtaka na kutuhoji, nao wakatutupa gerezani, hata ingawa sisi ni raia wa Rumi. Nao sasa wanataka kututoa gerezani kwa siri? Hapana! Wao na waje wenyewe watutoe humu gerezani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Paulo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, tena wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? Sivyo, lakini na waje wenyewe wakatutoe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Paulo akawaambia askari, “Wale maofisa hawakuthibitisha kuwa tulifanya chochote kibaya, lakini walitupiga kwa bakora hadharani na kutuweka gerezani. Nasi ni raia wa Rumi. Na sasa wanataka tuondoke kimya kimya. Haiwezekani, ni lazima waje hapa wao wenyewe kisha watutoe nje!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Paulo alimjibu, “Ati nini? Ingawa hatukuwa na kosa, walitupiga viboko hadharani hali sisi ni raia wa Roma. Tena, walitutia ndani na sasa wanataka kutufungulia kwa siri! Hata kidogo! Ni lazima wao wenyewe waje hapa watufungulie.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Paulo alimjibu, “Ati nini? Ingawa hatukuwa na kosa, walitupiga viboko hadharani hali sisi ni raia wa Roma. Tena, walitutia ndani na sasa wanataka kutufungulia kwa siri! Hata kidogo! Ni lazima wao wenyewe waje hapa watufungulie.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Paulo akawaambia wale maafisa, “Wametupiga hadharani bila kutufanyia mashtaka na kutuhoji, nao wakatutupa gerezani, hata ingawa sisi ni raia wa Rumi. Nao sasa wanataka kututoa gerezani kwa siri? Hapana! Wao na waje wenyewe watutoe humu gerezani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Paulo akawaambia wale maafisa, “Wametupiga hadharani bila kutufanyia mashtaka na kutuhoji, nao wakatutupa gerezani, hata ingawa sisi ni raiya wa Rumi. Nao sasa wanataka kututoa gerezani kwa siri? Hapana! Wao na waje wenyewe watutoe humu gerezani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Paulo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, tena wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? Sivyo, lakini na waje wenyewe wakatutoe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Paulo alimjibu, “Ati nini? Ingawa hatukuwa na kosa, walitupiga viboko hadharani hali sisi ni raia wa Roma. Tena, walitutia ndani na sasa wanataka kutufungulia kwa siri! Hata kidogo! Ni lazima wao wenyewe waje hapa watufungulie.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Paulo akawaambia: Wametupiga mbele ya watu pasipo kutuhukumu sisi tulio Waroma na kututia kifungoni. Sasa je? Wanataka kutukimbiza na kufichaficha? Sivyo, sharti waje wenyewe, watutoe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Paulo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, tena wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? Sivyo, lakini na waje wenyewe wakatutoe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Paulo akawaambia wajumbe: “Wametupiga mbele ya watu wote bila kutusambisha, ijapokuwa sisi ni wanainchi wa Roma, na kisha wakatutia ndani ya kifungo. Na sasa namna gani wanataka kututosha kwa uficho? Haiwezekani! Wao wenyewe wafike kutufungua!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Paolo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, teua wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? la, sivyo, na waje wenyewe wakatutoe.