Acts 17:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, Wayahudi wa Thesalonike walipogundua kwamba Paulo alikuwa anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo na kuchochea makundi ya watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wale Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kuwa Paulo anahubiri neno la Mungu huko Beroya, wakaenda huko ili kuwashawishi watu na kuwachochea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipojua kuwa Paulo alikuwa anawahubiri Ujumbe wa Mungu katika mji wa Berea, walikwenda huko pia. Waliwakasirisha watu na kufanya vurugu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, Wayahudi wa Thesalonika walipogundua kwamba Paulo alikuwa anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo na kuchochea makundi ya watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, Wayahudi wa Thesalonike walipogundua kwamba Paulo alikuwa anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo na kuchochea makundi ya watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wale Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kuwa Paulo anahubiri neno la Mungu huko Beroya, wakaenda huko nako wakishawishi watu na kuwachochea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wale Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kuwa Paulo anahubiri neno la Mungu huko Beroya, wakaenda huko ili kuwashawishi watu na kuwachochea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawavuruga na kuwafadhaisha makutano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, Wayahudi wa Thesalonike walipogundua kwamba Paulo alikuwa anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo na kuchochea makundi ya watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Wayuda wa Tesalonike walipotambua, ya kuwa Neno lake Mungu linatangazwa na Paulo hata huko Beroya, wakaja, wakawahangaisha watu nako huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Wayuda wa muji wa Tesalonika wakapata habari kwamba Paulo anahubiri Neno la Mungu vilevile katika muji Beroya. Kwa hiyo wakaenda kule, wakaanza kufanya fujo kati ya makundi ya watu na kuwachochea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini Wayahudi wa Thessaloniki walipopata khabari ya kwamba Neno la Mungu linakhubiriwa na Paolo katika Beroya, wakaenda huko wakawachafua makutano.