Acts 17:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na Timotheo walibaki Berea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara hiyo, wale ndugu wakamsafirisha Paulo hadi pwani, lakini Sila na Timotheo wakabaki Beroya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara hiyo wale ndugu wakampeleka Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakasalia huko.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo waamini walimpeleka Paulo sehemu za pwani, lakini Sila na Timotheo walibaki Berea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na Timotheo walibaki Berea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na Timotheo walibaki Berea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wale ndugu wa Beroya mara moja wakamsafirisha Paulo aende zake pwani, lakini Sila na Timotheo wakabaki Beroya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara hiyo, wale ndugu wakamsafirisha Paulo hadi pwani, lakini Sila na Timotheo wakabaki Beroya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara hiyo wale ndugu wakamtuma Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakabakia huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na Timotheo walibaki Berea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Papo hapo ndugu wakamsindikiza Paulo, wakamfikisha pwani. Lakini Sila na Timoteo wakakaa huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara hiyo wale ndugu wakampeleka Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakasalia huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu pale pale, wandugu waamini wakamusindikiza Paulo mpaka kwenye kivuko, lakini Sila na Timoteo wakabaki Beroya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra hiyo wale ndugu wakampeleka Paolo aende zake kana kwamba anakwenda njia ya pwani; bali Sila na Timotheo wakashinda huko.