Acts 17:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wengine waliofuata falsafa ya Epikuro na Stoiki walibishana naye. Wengine walisema, “Anataka kusema nini huyu bwanamaneno?” Kwa kuwa Paulo alikuwa anahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo, wengine walisema, “Inaonekana kama anahubiri juu ya miungu ya kigeni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kundi la wenye falsafa, Waepikureo na Wastoiko, wakajibizana naye. Baadhi yao wakasema, “Je, huyu mpayukaji anajaribu kusema nini?” Wengine wakasema, “Inaonekana anasema habari za miungu ya kigeni.” Walisema haya kwa sababu Paulo alikuwa anahubiri Injili kuhusu Isa na ufufuo wa wafu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wengine wakasema, Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya wanafalsafa Waepikureo na baadhi ya wanafalsafa Wastoiko walibishana naye. Baadhi yao walisema, “Mtu huyu hakika hajui anachokisema. Anajaribu kusema nini?” Paulo alikuwa anawaambia Habari Njema kuhusu Yesu na ufufuo. Hivyo walisema, “Anaonekana anatueleza kuhusu baadhi ya miungu wa kigeni.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wengine waliofuata falsafa ya Epikuro na Stoiki walibishana naye. Wengine walisema, “Anataka kusema nini huyu bwanamaneno?” Kwa kuwa Paulo alikuwa anahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo, wengine walisema, “Inaonekana kama anahubiri juu ya miungu ya kigeni.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wengine waliofuata falsafa ya Epikuro na Stoiki walibishana naye. Wengine walisema, “Anataka kusema nini huyu bwanamaneno?” Kwa kuwa Paulo alikuwa anahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo, wengine walisema, “Inaonekana kama anahubiri juu ya miungu ya kigeni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha baadhi ya Waepikureo na Wastoiko wenye elimu ya juu sana wakakutana naye. Baadhi yao wakasema, “Je, huyu mpayukaji anajaribu kusema nini?” Wengine wakasema, “Inaonekana anasema habari za miungu ya kigeni.” Walisema haya kwa sababu Paulo alikuwa anahubiri habari njema kuhusu Yesu na ufufuo wa wafu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha baadhi ya Waepikureo na Wastoiko wenye falsafa wakakutana naye. Baadhi yao wakasema, “Je, huyu mpayukaji anajaribu kusema nini?” Wengine wakasema, “Inaonekana anasema habari za miungu ya kigeni.” Walisema haya kwa sababu Paulo alikuwa anahubiri habari njema kuhusu Isa na ufufuo wa wafu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wengine wakasema, Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wengine waliofuata falsafa ya Epikuro na Stoiki walibishana naye. Wengine walisema, “Anataka kusema nini huyu bwanamaneno?” Kwa kuwa Paulo alikuwa anahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo, wengine walisema, “Inaonekana kama anahubiri juu ya miungu ya kigeni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kulikuwako wenye ujuzi wa chama cha Waepikurio na wa chama cha Wastoiko, wakabishana naye, wengine wakasema Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine tena wakasema: Anaonekana kuwa mtangazaji wa miungu migeni. Kwani alikuwa anawapigia hiyo mbiu njema ya Yesu na ya ufufuko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wengine wakasema, Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walimu wamoja wa kikundi cha Waepikurio na cha Wastoiko, wakaanza kubishana na Paulo. Wamoja wao wakauliza: “Huyu katetea anataka kusema nini?” Wengine wakasema: “Anaonekana kuwa muhubiri wa miungu ya kigeni.” Walisema hivi kwa sababu Paulo alikuwa akihubiri juu ya Yesu na jinsi alivyofufuka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo.