Acts 17:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturi yake, akajadiliana nao Sabato tatu mfululizo, akitumia Maandiko Matakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama ilivyokuwa desturi yake, Paulo aliingia ndani ya sinagogi, na kwa muda wa Sabato tatu akawa anahojiana nao kutoka kwa Maandiko,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo aliingia katika sinagogi kuwaona Wayahudi kama alivyokuwa akifanya. Wiki tatu zilizofuatia, kila siku ya Sabato alijadiliana nao kuhusu Maandiko.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturi yake akajadiliana nao Sabato tatu mfululizo, akatumia Maandiko Matakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturi yake, akajadiliana nao Sabato tatu mfululizo, akitumia Maandiko Matakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama desturi yake Paulo aliingia ndani ya sinagogi na kwa muda wa majuma matatu akawa anahojiana nao kutoka kwenye Maandiko
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama desturi yake, Paulo aliingia ndani ya sinagogi, na kwa muda wa Sabato tatu akawa anahojiana nao kutoka kwenye Maandiko,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimokuwa, akahojiana nao kwa maneno ya Maandiko sabato tatu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturi yake, akajadiliana nao Sabato tatu mfululizo, akitumia Maandiko Matakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama Paulo alivyozoea, akaingia humo, akaongea nao maneno ya Maandiko siku tatu za mapumziko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sawa ilivyokuwa desturi, Paulo akaingia katika nyumba ile. Kwa muda wa siku tatu za Sabato zilizofuatana juma kwa juma, akabishana na watu waliokuwa mule, akitumia Maandiko Matakatifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Paolo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahujiana nao kwa maneno yii maandiko sabato tatu,