Acts 17:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
maana nilipokuwa napita huko na huko nikiangalia sanamu zenu za ibada niliona madhabahu moja ambayo imeandikwa: ‘Kwa Mungu asiyejulikana.’ Basi, huyo mnayemwabudu bila kujua, ndiye ninayemhubiri kwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini na kuangalia kwa makini vitu vyenu vya kuabudiwa, niliona huko madhabahu moja iliyoandikwa: Kwa Mungu Asiyejulikana.Basi sasa kile ambacho mmekuwa mkikiabudu kama kisichojulikana, ndicho ninachowahubiria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilikuwa natembea katika mji wenu na nimeona mambo mnayoyaabudu. Niliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya juu yake: ‘KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.’ Mnamwabudu mungu msiyemjua. Huyu ni Mungu ninayetaka kuwaambia habari zake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sababu yenyewe ni kwamba katika pitapita yangu niliangalia sanamu zenu za ibada nikakuta madhabahu moja ambayo imeandikwa: Kwa ajili ya Mungu yule Asiyejulikana. Basi, huyo mnayemwabudu bila kujua, ndiye ninayemhubiri kwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
maana nilipokuwa napita huko na huko nikiangalia sanamu zenu za ibada niliona madhabahu moja ambayo imeandikwa: ‘Kwa Mungu asiyejulikana.’ Basi, huyo mnayemwabudu bila kujua, ndiye ninayemhubiri kwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini na kuangalia kwa bidii vitu vyenu vya kuabudiwa, niliona huko madhabahu moja iliyoandikwa: KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi sasa kile ambacho mmekuwa mkikiabudu kama kisichojulikana, ndicho ninachowahubiria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini na kuangalia kwa bidii vitu vyenu vya kuabudiwa, niliona huko madhabahu moja iliyoandikwa: kwa mungu asiyejulikana. Basi sasa kile ambacho mmekuwa mkikiabudu kama kisichojulikana, ndicho ninachowahubiria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu nilipokuwa nikipita huku na huko na kuyaona mambo ya ibada zenu, niliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
maana nilipokuwa napita huko na huko nikiangalia sanamu zenu za ibada niliona madhabahu moja ambayo imeandikwa: ‘Kwa Mungu asiyejulikana.’ Basi, huyo mnayemwabudu bila kujua, ndiye ninayemhubiri kwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nilipozunguka na kupatazama pa kuombea penu nikaona pa kuchinjia ng'ombe za tambiko palipoandikwa: Penye Mungu asiyetambulikana. Basi, huyo, mnayemtumikia pasipo kumjua, ndiye, ninayewatangazia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana nilipokuwa nikipitapita katika muji wenu nilichunguza nafasi zenu za kuabudia, nikaona hata mazabahu mamoja ambako waliyochora maandiko haya: ‘Kwa ajili ya mungu asiyejulikana.’ Basi yule munayemwabudu pasipo kumujua ndiye mimi ninayemuhubiri kwenu sasa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona maabudu yenu, naliona madhliahu iliyoandikwa maneno haya, Kwa Mungu yule asiyejulikana. Bassi mimi nawakhubirini khabari zake yeye ambae ninyi mnamwabudu hila kumjua.