Acts 17:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na dunia; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo, ndiye Bwana wa mbingu na nchi; hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni Mungu aliyeumba ulimwengu na kila kitu ndani yake. Ni Bwana wa mbingu na nchi. Haishi katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya kibinadamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na nchi; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na dunia; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwenyezi Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na dunia; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu aliyeuumba ulimwengu navyo vyote vilivyomo hakai katika nyumba za kuombea zilizojengwa na mikono ya watu, kwani yeye ni Bwana wa mbingu na wa nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vinavyokuwa ndani yake, yeye anayekuwa Bwana wa mbingu na dunia, hakai ndani ya hekalu zilizojengwa na watu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na inchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono: