Acts 17:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliyaeleza na kuonesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka kutoka kwa wafu. Akawaambia, “Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akidhihirisha wazi na kuthibitisha kwamba ilikuwa lazima Al-Masihi ateswe na afufuke kutoka kwa wafu. Akasema, “Huyu Isa ninayewaambia habari zake, ndiye Al-Masihi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alifafanua Maandiko kuwaonesha kuwa Masihi ilikuwa afe na kufufuka kutoka kwa wafu. Aliwaambia, “Huyu Yesu ninayewaambia habari zake ndiye Masihi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Aliyaeleza na kuonyesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka kutoka wafu. Akawaambia, “Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliyaeleza na kuonesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka kutoka kwa wafu. Akawaambia, “Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akidhihirisha wazi na kuthibitisha kwamba ilikuwa lazima Kristo ateswe na afufuke kutoka kwa wafu, akasema, “Huyu Yesu ninayewaambia habari zake, ndiye Kristo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akidhihirisha wazi na kuthibitisha kwamba ilikuwa lazima Al-Masihi ateswe na afufuke kutoka kwa wafu. Akasema, “Huyu Isa ninayewaambia habari zake, ndiye Al-Masihi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewaambia ninyi habari zake ndiye Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliyaeleza na kuonesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka kutoka kwa wafu. Akawaambia, “Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawafunulia na kuwaelezea, ya kuwa Kristo alipaswa na kuteswa na kufufuka katika wafu, akawaambia: Yesu, ambaye ninawatangazia habari zake, yuyu huyu ndiye Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliwaelezea na kuwaonyesha wazi kwamba Kristo alipaswa kuteswa na kufufuka. Akawaambia: “Huyu Yesu ninayemuhubiri kwenu ndiye Kristo.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kama, Yesu huyu ninaewapasha ninyi khabari zake ndiye Kristo.