Acts 17:34 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu kadhaa waliandamana naye, wakawa waumini. Miongoni mwao walikuwa Dionisio wa Areopago, na mwanamke mmoja aitwaye Damari na wengineo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini baadhi yao wakaungana naye wakaamini. Kati yao walikuwemo Dionisio, mmoja wa mkutano wa Areopago, na mwanamke mmoja aliyeitwa Damari, na wengine wengi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baadhi ya watu wakashikamana naye, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini baadhi ya watu waliungana na Paulo na kuwa waamini. Miongoni mwao walikuwa Dionisi, ambaye alikuwa mjumbe wa baraza la Areopago, na mwanamke aliyeitwa Damari na baadhi ya wengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini watu kadhaa waliandamana naye, wakawa waumini. Miongoni mwao walikuwa Dionisio wa Areopago, mwanamke mmoja aitwaye Damari na wengineo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu kadhaa waliandamana naye, wakawa waumini. Miongoni mwao walikuwa Dionisio wa Areopago, na mwanamke mmoja aitwaye Damari na wengineo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini baadhi yao wakaungana naye wakaamini. Kati yao alikuwepo Dionisio, Mwareopago na mwanamke mmoja aliyeitwa Damari na wengine wengi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini baadhi yao wakaungana naye wakaamini. Kati yao alikuwepo Dionisio, Mwareopago na mwanamke mmoja aliyeitwa Damari na wengine wengi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baadhi ya watu wakaungana naye, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu kadhaa waliandamana naye, wakawa waumini. Miongoni mwao walikuwa Dionisio wa Areopago, na mwanamke mmoja aitwaye Damari na wengineo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walikuwako waliogandamana naye, wakaja kumtegemea Bwana. Miongoni mwao alikuwamo mtu wa Areopago, ndiye Dionisio, tena mwanamke, jina lake Damari, na wengine waliokuwa pamoja nao.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baadhi ya watu wakashikamana naye, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa vile watu wamoja walijiunga naye na kuamini. Kati yao kulikuwa Dionisio, mumoja wa Baraza Kubwa inayoitwa Areopago, pamoja na mwanamuke mumoja aliyeitwa Damari na watu wengine vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baadhi ya wanaume wakashikamana nae, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionuso, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao.