Acts 17:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadhi yao walikubali wakajiunga na Paulo na Sila. Kadhalika, idadi kubwa ya Wagiriki waliomcha Mungu pamoja na wanawake wengi wa tabaka la juu, walijiunga nao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadhi ya Wayahudi wakasadiki, wakaungana na Paulo na Sila, wakiwepo idadi kubwa ya Wayunani waliomcha Mungu na wanawake wengi mashuhuri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya Wayahudi pale waliwaamini Paulo na Sila na waliamua kujiunga nao. Idadi kubwa ya Wayunani waliokuwa wanamwabudu Mungu wa kweli na wanawake wengi maarufu walijiunga nao pia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baadhi yao walikubali wakajiunga na Paulo na Sila. Kadhalika, idadi kubwa ya Wagiriki waliomcha Mungu pamoja na wanawake wengi wa tabaka la juu, walijiunga nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadhi yao walikubali wakajiunga na Paulo na Sila. Kadhalika, idadi kubwa ya Wagiriki waliomcha Mungu pamoja na wanawake wengi wa tabaka la juu, walijiunga nao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya Wayahudi wakasadiki, wakaungana na Paulo na Sila, wakiwepo idadi kubwa ya Wayunani waliomcha Mungu na wengi wa wanawake mashuhuri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadhi ya Wayahudi wakasadiki, wakaungana na Paulo na Sila, wakiwepo idadi kubwa ya Wayunani waliomcha Mungu na wanawake wengi mashuhuri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wengine miongoni mwao wakaamini, wakafuatana na Paulo na Sila; na Wagiriki waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadhi yao walikubali wakajiunga na Paulo na Sila. Kadhalika, idadi kubwa ya Wagiriki waliomcha Mungu pamoja na wanawake wengi wa tabaka la juu, walijiunga nao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wamoja wao wakashindwa mioyoni, wakashikamana nao akina Paulo na Sila; nao waliotoka kwa Wagriki wenye kumcha Mungu walikuwa wengi mno, hata wanawake wenye cheo hawakuwa wachache.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wamoja kati ya Wayuda wakasadiki na kujiunga pamoja na Paulo na Sila. Vilevile kundi kubwa la Wagriki walioogopa Mungu pamoja na wanawake wengi wenye heshima wakasadiki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wengine wakaamini, wakasuhubiana na Paolo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye eheo si wachache.