Acts 17:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Wayahudi wakaona wivu; wakawakodi wafidhuli sokoni, wakafanya kikundi na kuzusha fujo mjini kote. Wakaivamia nyumba ya Yasoni wakitumaini kuwapata humo Paulo na Sila ili wawalete hadharani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Wayahudi ambao hawakuwa wameamini wakawa na wivu, wakawakodi watu waovu kutoka sokoni, wakakutanisha umati wa watu, wakaanzisha ghasia mjini. Wakaenda mbio nyumbani mwa Yasoni wakiwatafuta Paulo na Sila ili kuwaleta nje penye umati ule wa watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Wayahudi ambao hawakuamini wakaingiwa na wivu, hivyo wakawakusanya baadhi ya watu wabaya katikati ya mji ili kufanya vurugu. Wakaunda kundi na wakanzisha vurugu mjini. Walikwenda nyumbani kwa Yasoni kuwatafuta Paulo na Sila. Walitaka kuwaleta mbele ya watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Wayahudi wakaona wivu; wakawakodi wafidhuli sokoni, wakafanya kikundi na kuzusha fujo mjini kote. Wakaivamia nyumba ya Yasoni wakitumaini kuwapata humo Paulo na Sila ili wawalete hadharani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Wayahudi wakaona wivu; wakawakodi wafidhuli sokoni, wakafanya kikundi na kuzusha fujo mjini kote. Wakaivamia nyumba ya Yasoni wakitumaini kuwapata humo Paulo na Sila ili wawalete hadharani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Wayahudi ambao hawakuwa wameamini wakawa na wivu, wakawakodi watu waovu kutoka sokoni, wakakutanisha umati wa watu, wakaanzisha ghasia mjini. Wakaenda mbio nyumbani kwa Yasoni wakiwatafuta Paulo na Sila ili kuwaleta nje penye ule umati wa watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Wayahudi ambao hawakuwa wameamini wakawa na wivu, wakawakodi watu waovu kutoka sokoni, wakakutanisha umati wa watu, wakaanzisha ghasia mjini. Wakaenda mbio nyumbani kwa Yasoni wakiwatafuta Paulo na Sila ili kuwaleta nje penye ule umati wa watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadhaa miongoni mwa watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Wayahudi wakaona wivu; wakawakodi wafidhuli sokoni, wakafanya kikundi na kuzusha fujo mjini kote. Wakaivamia nyumba ya Yasoni wakitumaini kuwapata humo Paulo na Sila ili wawalete hadharani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Wayuda wakaingiwa na wivu, wakajichukulia kikundi cha majitu mabaya wasiokuwa na kazi; hao wakakusanya kundi zima la watu, kisha wakauchafua mji wote, wakaisogeleasogelea nyumba ya Yasoni, wakawatafuta, wawapeleke kwenye kundi lilelile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Wayuda wakajaa na wivu, hata wakakusanya watu wamoja wa ovyo ovyo waliowakuta kwenye nafasi za makutano, na kufanya kikundi. Kisha wakafanya fujo katika muji wote. Wakashambulia nyumba ya Yasoni, wakiwatafuta Paulo na Sila kusudi wawapeleke mbele ya watu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;