Acts 18:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakasema, “Tunamshtaki mtu huyu kwa sababu ya kuwashawishi watu wamwabudu Mungu kwa namna inayopingana na sheria.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamshtaki wakisema, “Mtu huyu anawashawishi watu wamwabudu Mungu kinyume cha sheria.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakisema Mtu huyu huwavuta watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakamwambia Galio, “Mtu huyu anawafundisha watu kumwabudu Mungu kwa namna ambavyo ni kunyume na sheria yetu!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakasema, “Tunamshtaki mtu huyu kwa sababu ya kuwashawishi watu wamwabudu Mungu kwa namna inayopingana na Sheria.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakasema, “Tunamshtaki mtu huyu kwa sababu ya kuwashawishi watu wamwabudu Mungu kwa namna inayopingana na sheria.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamshtaki wakisema, “Mtu huyu anawashawishi watu wamwabudu Mungu kinyume cha sheria.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamshtaki wakisema, “Mtu huyu anawashawishi watu wamwabudu Mwenyezi Mungu kinyume cha sheria.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakisema Mtu huyu huwashawishi watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakasema, “Tunamshtaki mtu huyu kwa sababu ya kuwashawishi watu wamwabudu Mungu kwa namna inayopingana na sheria.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakasema: Huyu anawahimiza watu kumcha Mungu na kuyabeza Maonyo yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakisema Mtu huyu huwavuta watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kumushitaki: “Mutu huyu anawavuta watu kumwabudu Mungu kwa njia isiyopatana na Sheria yetu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakisema, Mtu huyu huwavuta watu illi wamwabudu Mungu kinyume cha sharia yetu.