Acts 18:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kukaa huko kwa muda, akaondoka na kwenda sehemu moja hadi nyingine huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha wanafunzi wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya nchi ya Galatia na Frigia, mji kwa mji, akiwathibitisha wanafunzi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikaa Antiokia kwa muda kisha akaondoka akipita katika nchi za Galatia na Frigia. Alisafiri kutoka mji mmoja hadi mji mwingine katika mikoa hii, akiwasaidia wafuasi wa Yesu kuimarika katika imani yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kukaa huko kwa muda, akaondoka na kwenda kutoka sehemu moja hadi nyingine huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha wanafunzi wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kukaa huko kwa muda, akaondoka na kwenda sehemu moja hadi nyingine huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha wanafunzi wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya kukaa huko kwa siku kadhaa akaondoka, akapita kati ya nchi ya Galatia na Frigia, mji kwa mji, akiwatia moyo wanafunzi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kukaa huko siku kidogo akaondoka tena, akakata nchi ya Galatia na ya Furigia na kuingia mji kwa mji akiwashupaza wanafunzi wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya nchi ya Galatia na Frigia, mji kwa mji, akiwathibitisha wanafunzi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipokwisha kukaa Antiokia kwa siku chache, akaondoka kule, akapita muji kwa muji toka katika inchi ya Galatia mpaka katika inchi ya Furigia, na kule akawatia wanafunzi nguvu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya inchi ya Galatia na Frugia, mji kwa mji, akiwatia moyo wanafunzi.