Acts 18:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa Maandiko Matakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi akaja Efeso Myahudi aliyeitwa Apolo, mzawa wa Iskanderia. Alikuwa na elimu kubwa, pia alikuwa na ujuzi wa Maandiko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Myahudi aliyeitwa Apolo alikuja Efeso. Alizaliwa katika mji wa Iskanderia, alikuwa msomi aliyeyajua Maandiko vizuri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa Maandiko Matakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa Maandiko Matakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi akaja Efeso Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mwenyeji wa Aleksandria. Yeye alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kunena, pia alikuwa hodari katika maandiko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi akaja Efeso Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mwenyeji wa Iskanderia. Yeye alikuwa na elimu kubwa, pia alikuwa hodari katika Maandiko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, msemaji mzuri, akafika Efeso; naye alikuwa na ujuzi wa Maandiko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa Maandiko Matakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulikuwa na Myuda, jina lake Apolo, aliyezaliwa Alekisandria; alikuwa na nguvu ya kusema, tena nguvu yake ilitoka katika utambuzi wa Maandiko; naye akafika Efeso.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku zile, Muyuda mumoja, jina lake Apolo, muzaliwa wa muji Alesanduria, alikuwa amefika katika muji Efeso. Alikuwa mutu mwenye uwezo katika masemi na mwenye kuelewa sana Maandiko.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Myahudi mmoja, jina lake Apollo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akalika Efeso; nae alikuwa hodari wa maandiko.