Acts 18:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana Isa, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi kuhusu Isa, ingawa alijua tu ubatizo wa Yahya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwa amefundishwa kuhusu Bwana na daima alifurahia kuwaeleza watu kuhusu Yesu. Alichofundisha kilikuwa sahihi, lakini ubatizo alioufahamu ni ubatizo aliofundisha Yohana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu. Akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi juu ya Yesu, ingawa alijua tu ubatizo wa Yohana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana Isa, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi juu ya Isa, ingawa alijua tu ubatizo wa Yahya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa bidii habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana, akashurutishwa na Roho kusema na kuyafundisha mambo ya Yesu, yalivyo kweli, lakini aliujua ubatizo wa Yohana tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu huyu alikuwa amefundishwa Njia ya Bwana, naye alitangaza kwa bidii sana na kufundisha kwa ukweli habari za Yesu. Lakini alikuwa akijua tu ubatizo wa Yoane.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu huyu alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikiwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi khabari za Bwana; nae alijua ubatizo wa Yohana tu.